Jamaa kanunua mashine kaipeleka nyumbani. Kazi ya mashine hiyo nh kila ukisema uongo inagundua ni uongo na inakukandamiza makofi hapo hapo.
Wakati wa msosi wa usiku jamaa akaileta mashine imekaa kama roboti, akaiweka karibu na meza
Akaanza: Mwanangu, leo wakati wa shule ulikuwa wapi?
Mtoto akajibu: nilikuwa shule baba (Twaaaaaaaap mashine ikambamiza makofi).
Samahani baba ila kwa kweli nilienda kuangalia sinema kwa kina Mudi.
Dingi: Sinema gani?
Mtoto: Aki na Ukwa (Twaaaaaaaap, mashine ikambamiza makofi).
Samahani baba kiu kweli ilikuwa ni sinema ya popobawa.
Dingi: toto pumbavu sana, enzi zangu mimi hata sikutamani kuangalia picha hizo za kijinga (Twaaaaaaaaap mashine ikambamiza dingi makofi).
Mama akaingilia huku anacheka: Hahahahaha, ndo mtoto wako huyo (Twaaaaaa--ap mashine ikampiga mama makofi)
0 comments