Sunday, 9 June 2013

COASTAL AMKENI

KIKOSI CHA COASTAL KATIKA MOJA YA MICHEZO YAO KATIKA UWANJA WA TAIFA MSIMU ULIOPITA
Na Abdallah H.I Sulayman

Msimu wa 2011/12 mabingwa wa Tanzania bara mwaka 1988 Coastal Union waliuwanza msimu vibaya kiasi kwamba ika pelekea mzunguko wa kwanza kwisha wakiwa katika eneo la kushuka daraja.

Hali hiyo ilipelekea wakiazi wa Tanga kufanya juhudi kuhakikisha timu yao ya Coastal aishuki daraja na kupata sapoti kubwa toka kwa mfanyabiashara mashuhuri toka katika mji wa Tanga Nassor Binslum na wengineo kuhakikisha Coastal haishuki daraja na msimu ujao kurejesha makali yao ya miaka ya nyuma.

Coastal walifanikiwa kusalia kwenye ligi huku wakimaliza katika nafasi 5 za juu katika msimu huo na kunza kufanya usajili wa kuhakikisha msimu uliomalizika (2012/13) wakimaliza katika nafasi 3 za juu.

Walimrejesha kiungo toka Kenya Jerry Santos nchini huku wakimpatia mkataba mshambuliaji Selemani Kasimj Selembe na Nsa Job, wote kwa pamoja na wengine waliiwezesha Coastal kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa katuika 4 bora lakini wakamaliza ligi wakiwa katika nafasi ya 6.

Coastal union wakiwa bado na dhamira yao teyari wamesha sajili nyota wengine kwa ajili ya msimu ujao akiwemo kiungo kipenzi cha mashabiki wa Simba Haruna Moshi Boban, sambamba na beki Juma Nyosso kwa ajili ya msimu juao.

Sio kusudio langu leo kuzungumzia namna Coastal wanavyojiandaa kurejesha heshima ya jiji la Tanga na klabu yenyewe ila dhumuni langu kuwashtua viongozi wa Coastal kutumia fursa hii ya kupata sapoti toka kwa wadau wa jiji la Tanga.

Huu ni wakati wa Coastal kuingia mikataba na wadhamini mbalimbali, huku wakiboresha na kutafuta vyanzo vingine vya mapato.

Viongozi wa coastal union wasilizike nha ufadhili wa Binslum, bali watumie fursa hii ya wakazi wa Tanga kujitokeza katika michezo yao kuwashawishi wadhamini wengine.


0 comments