Mkalimani wa lugha ya Kichina , Dk Rashied Kabongo ( kulia) akitoa tafsiri ya lugha ya kichina kwa kishwahili kutoka kwa Mkurugenzi Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius
ya China, Tong Jun ,wakati alipokuwa akitoa shukrani zake kwa Viongozi
wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro na Serikali ya Mkoa mara baada ya
uzinduzi wa mpango wa ufundishaji wa lugha ya kichina Chuoni hapo,
tayari Taasisi hiyo inafundisha lugha hiyo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
na Dodoma.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Waislamu Morogoro, Profesa Hamza Njozi akitoa hotuba ya utangulizi.
Baadhi ya wanachuo cha MUM.
Wakisikiliza Hotuba.
Mmoja wa wakufunzi wa Taasisi ya Confucius ya China inayofundisha lugha ya kichina hapa
nchini , Wei Jianli ‘ Bi Shuxia’ ,akisikiliza moja ya swali kutoka kwa
mwanafunzi mmoja wapo wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro akitaka kujua
baadhi ya vitu vilivyopo mezani kwa maneno ya kichina , Nov 2, mwaka
huu baada ya uzinduzi wa mpango wa ufundishaji wa lugha ya kichina
Chuoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi ( watano kushoto),katika
picha ya pamoja na Viongozi wa MUM na Taasisi ya Confucius ya China
inayofundisha lugha ya kichina Chuoni hapo.( Picha na John Nditi).
0 comments