Mkoa wa Tanga upo kwenye mchakato wa kurasimisha bandari bubu
tatu ili zipandishwe hadhi na kufanya kazi chini uangalizi wake, tofauti
na sasa zinatumika kupitisha biashara za magendo na wahamiaji haramu.
Akizungumza na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili
na Mazingira juzi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa alisema bandari
hizo bubu zinatumika vibaya, hivyo ni bora zikatambuliwa ili kuingiza
mapato serikalini.
Gallawa alitaja bandari hizo kuwa ni Jasini
iliyopo wilaya ya Mkinga, Kigombe wilayani Muheza na Kipumbwi iliyopo
Pangani na kwamba, hizo ni kati ya 40 zilizopo Tanga.
Alisema baada ya kuzitembelea na kukagua shughuli
zinazofanyika kila siku, Serikali imebaini bandari hizo bubu zinavusha
bidhaa mbalimbali. Pia, zinatumika kama milango ya kuingia kutoka maeneo
mbalimbali duniani.
Mwenyeikiti wa kamati hiyo, James Lembeli
alipongeza Mkoa kwa kuchukua hatua hiyo, kwani siku zilizopita
zilikamatwa meno ya tembo nje ya nchi na kubainika kuwa zimepitia mkoani
hapa.
0 comments