Dawa ambayo kwa kawaida hutumika kupunguza makali ya
virusi vya UKIMWI imegunduliwa kuwa ina uwezo wa kutibu Saratani ya
kizazi vikamilifu baada ya kipindi cha miezi mitatu katika utafiti
uliofanywa Hospitali kuu ya Kenyatta nchini Kenya.
Miezi mitatu baadaye zaidi ya asilmia 90 ya wagonjwa hao walipatikana kupona kutokana na ugonjwa huo wa Saratani.
Taarifa ya chuo kikuu cha Manchester ilisema kuwa kati ya wanawake 23 waliotambuliwa kuugua ugonjwa huo wenye makali zaidi, 19 waliweza kurudi katika hali yao ya afya ya kawaida na kwa wawili makali ya Saratani yalionekana kupungua.
Wanawake 17 wengine ambao pia waligunduliwa kuwa na ugonjwa huo ambao ulikuwa katika awamu ya kwanza, walipata buheri wa afya kama wenzao.
Ugunduzi wa utafiti huo ambao uliibua mjadala mkali katika chuo kikuu cha Manchester, iwapo ni ukweli, ni wa kushangaza na huenda ukawa ni miujiza katika matibabu ya Saratani ya kizazi miongoni mwa nchi zinazoendelea.
Pindi tu mtu anapogunduliwa kuwa na ugonjwa huo, mgonjwa anapaswa kumeza tembe moja ya dawa ya kupunguza makali ya UKIMWI mara mbili kila siku kwa muda wa majuma mawili.
chanzo: bbc swahili
0 comments