Sunday, 16 March 2014

POLISI KENYA YAANZA MSAKO KWA WALIOMPIGA SHEIKH ALI BAHERO

By    
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEicxA1Qhs190kjpcy74H1hCGEBXyQu8QSWR_uIfPV3EvYvJDcpXMRaYg6l7I8c5d59xpbYg7MecuFYTgSZLU5ppvwJRi9zyf-rnZ2CeDcnYQ31pyAheryQhmMQPzQV4C1Z4CA1GZ6TYVkEb/s1600/bahero.JPG

Polisi mjini Mombasa wameanzisha msako wa vijana 40 ambao asubuhi ya Alhamisi Machi 13 walitumia mawe na vitu kumshambulia Sheikh Ali Bahero kwenye eneo la Majengo baada ya kuripotiwa kukosana na vijana hao wanaolalamika.

Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Mombasa, Geoffrey Mayek, alisema polisi walikwenda kufuatilia ripoti ya tukio moja kwenye Chuo cha Gateaway na walipofika wakampata Sheikh Ali Bahero, msaidizi wa zamani wa Sheikh Aboud Rogo, Mohammed, wakiwa wameloa damu, liliripoti gazeti la Daily Nation la Kenya.


Sheikh Bahero alinusurika kifo Alhamis saa 3 asubuhi baada ya kushambuiwa kwa Visu, mawe na genge la Vijana wenye hasira dhidi yake akielekea Ofisini kwake katika mtaa wa majengo mjini mombasa.

Vijana hao wamemshambulia Bahero kwa kumtuhumu kuwa anafundisha itikadi isiyo sahihi (Itikadi ya Kupinga Da'awah Jihaad). 
  Bahero alipelekwa Hospitali ya Jocham ambako anasemekana kuwa katika hali nzuri.

"Hadi sasa hakuna aliyekamatwa kwani vijana hao walikimbia lakini tumeanzisha uchunguzi juu ya suala hilo," alisema Mayek. "Pia tutachukua maelezo kutoka kwa sheikh huyo mara tu atakapoweza kuzungumza nasi."

Washukiwa hao waliripotiwa kumshambulia pia mwalimu mkuu wa shule ambaye alijaribu kuingilia kati kumuokoa Sheikh Bahero.

"Tunashuku kwamba vijana hao waliomshambulia Sheikh Bahero wamepandikizwa siasa kali lakini bado ni mapema kwangu mimi kuwaunganisha na ghasia za Masjid Mussa," aliongeza Mayek, akikusudia makabiliano yaliyomwaga damu kati ya polisi na vijana wanaoshukiwa kupandikizwa siasa kali kwenye msikiti huo mapema mwezi wa Februari.

Bahero hufundisha kwenye Madrasa Fathil Adhym na madrasa nyengine Kisauni, 

SOURCE: aHBAABUR RASUL

0 comments