Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe
Samia Sululu Hassan akifungua warsha ya siku moja kwa wahariri na waandishi
wa habari juu ya nafasi ya watetezi wa Haki za Binadamu katika Katiba
mpya.
.waambiwa waache kamari ya majongoo kuhusu serikali mbili
ama tatu
.watetezi wa haki za binadamu, waandishi watoswa kwenye
rasimu ya Katiba
Na
Damas Makangale, Dodoma, MOblog
WAANDISHI na Wahariri wa vyombo vya habari nchini
wamehimizwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na kuweka mbele
maslahi ya taifa wakati wa kuripoti Bunge maalum la katiba. MOblog
inaripoti.
Akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari
kuhusu nafasi ya watetezi wa haki za binadamu na asasi za kirai katika
katiba mpya jijini Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe
Samia Sululu Hassan amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya
kuelimisha jamii juu ya haki za binadamu kupitia kalamu zao kwa kuzingatia
weledi wa fani yao na maadili ya uandishi.
"waandishi wa habari pamoja na wahariri wao wanaweza kwa
kuweka mbele maslahi ya taifa kuripoti na kuandika habari zenye kuleta
suluhu, amani, mshikamano na utulivu," amesema.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
(THRDC), Ndg. Onesmo Olengurumwa akitoa mada juu ya ya mtazamo na jukumu la
wabunge wa katiba na waandishi wa habari za katiba pamoja na watetezi wa
haki za binadamu katika mchakato wa kuandika Katiba mpya mkutano wa siku
moja uliofanyika mjini Dodoma.
Amesema waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao
wanaweza kushauri na kushirikiana na serikali na mamlaka zingine kupatikana
kwa katiba mpya yenye tunu za taifa,
Sululu
aliongeza kwa kuweka hoja zao kwa ari ya utulivu wanaweza kabisa kuleta
mshikamano na ushirikiano wa kitaifa katika kudumisha amani na haki za
binadamu nchini.
Amesema kwamba kupitia bunge la katiba wanahabari ni
kiungo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa wananchi na kuelimisha umma jinsi
sheria na haki za binadamu zinavyoweza kulinda na katiba ya
nchi.
Mwezeshaji, Mwandishi wa Habari, Mwanasheria, msomi
na mjumbe wa Bunge la Katiba Ali Uki akizungumza kwenye warsha
hiyo.
"waandishi kwa kutumia nafasi yao wanaweza kushauri kwa
kurekebishwa baadhi ya sheria, vifungu ili kuweza kulinda haki za binadamu
nchini kwa kupitia bunge maalum la katiba," aliongeza.
Alisisitiza Mhe Sululu kwamba bunge la katiba halijadili
kuhusu ama serikali mbili au tatu kwa sababu kuna mambo mengi kwenye rasimu
ya katiba yakujadiliwa.
"kwa
jinsi mnavyoripoti kuhusu serikali mbili ama tatu ni kama mchezo wa kamari
ya majongoo jamani katiba siyo muungano tu," amesema.
Kwa
upande, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo
olengurumwa amesema ingawaje kwenye rasimu ya katiba hawajatambua watetezi
wa haki za binadamu bali wataendelea kushauriana na wajumbe kupata mwafaka
wa jambo hilo.
Meza kuu, Ndg. Onesmo Olengurumwa akiwa na Mgeni
rasmi Samia Suluhu Hassani kwenye warsha hiyo.
"Rasimu ya katiba haijatambua mahali popote nafasi ya
mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki mbali mbali za raia kama
zilivyoanishwa kikatiba," amesema
Olengurumwa aliongeza kwamba rasimu ya katiba pia
haijatambua wasaidizi wa kisheria wakujitolea (Paralegal) ambao wanatoa
msaada mkubwa kisheria kwenye ngazi za vijijini.
Amesema ni muhimu kwa watanzania kuendelea kupanua
mjadala wa katiba ili misingi ya haki za binadamu iingie kwenye mifumo ya
utetezi wa haki za binadamu nchini.
Olengurumwa amesema waandishi wa habari kama vile
watetezi wa haki za binadamu maisha yao lazima yalindwe na kutetewa na
katiba ya nchi ili kujenga mazingira mazuri ya haki za binadamu
nchini.
Hivi
karibuni rasimu ya pili ya Katiba ilipendekeza Muungano wa Serikali tatu -
Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali
ya Tanganyika.
Mjadala wake ulianza, ambapo wasomi walikosoa takwimu za
Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa
zimetumika kuupotosha umma.
wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato
Nyamsenda na Bashiru Ally wakati wakizungumza katika kipindi cha Je,
Tutafika? kinachorushwa na Channel Ten hivi karibuni.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo waandishi na
wahariri kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Nyamsenda amesema ukweli wa takwimu hizo uko kwenye
ripoti ya Tume hiyo, ambayo haipatikani kwa urahisi huku watu wakiishia tu
kusoma tu rasimu ambayo haielezi majukumu waliyopewa, mahali walipopita,
idadi ya wananchi na maoni yao.
Takwimu za Tume
Akifafanua zaidi, Nyamsenda anasema takwimu zinazotajwa
kwamba asilimia 61 ya Watanzania Bara wanataka Serikali tatu, asilimia 60
ya Wazanzibari wanataka Serikali ya Mkataba si za kweli.
"Tume
ya Warioba imetoa takwimu kuwa, watu waliotoa maoni kwa jumla ni 333,537.
Kati yao, waliogusia Muungano ni 77,000, kwa hiyo 256,537 hawakugusia
Muungano," anasema na kuongeza:
"Ukiwagawanya katika Bara utakuta ni watu wapatao 36,000
na Visiwani watu 38,000. Kati ya waliozungumzia muungano. Kwa Zanzibar watu
19,000 hawakugusia muundo na watu 10,400 ndiyo waligusia Muungano wa
Mkataba."
Anaendelea kufafanua: "Waliozungumzia Serikali mbili ni
6,460 sawa na asilimia 34. Kwa hiyo ni wachache kuliko waliozungumzia
Serikali ya Mkataba ambao nao ni wachache kuliko wale ambao hawakugusia
kabisa suala la muungano. Ni sawa na tone la maji katika bahari,"
amesema.
Benedict Ishabakaki, Afisa Usalama wa Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu akishiriki mkutano
huo.
Anaendelea kufafanua kuwa waliotoa maoni kuhusu Serikali
ya Mkataba na Serikali tatu, ni wachache huku wengi wakiwa
Bara.
"Kama
jumla ya watu waliotoa maoni ya Katiba ni 333,537, huwezi ukachukua watu
16,000 waliotaka Serikali tatu ukawaziba wengi ambao hawakutaka," anasema
na kuongeza:
"Ukijumlisha watu wanaotaka Serikali moja na mbili ambao
ni 16,475, utaona ni wengi kuliko wanaotaka Serikali tatu ambao ni
16,470."
Anasema watu hao wakiwekwa katika kundi ambalo
halikugusia kabisa muundo wa muungano, ni watu 287,537 sawa na asilimia
86.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki
wa warsha hiyo ya siku moja.
0 comments