WIZARA ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imeandaa miswada ya
sheria za matumizi salama ya mtandao ili kukabiliana na uhalifu kwa
njia ya mtandao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Wizara na Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano, Prisca Ulomi, alisema wizara imefikia hatua hiyo kutokana na changamoto mbalimbali.
Alisema miswada hiyo ni ya sheria ya kulinda Taarifa Binafsi, Sheria ya Biashara, Miamala ya Ki-elektroniki pamoja na muswada wa Sheria ya kuzuia uhalifu kwa njia ya kompyuta na mtandao.
“Sote kwa pamoja tumeshuhudia ukuaji wa kasi na mabadiliko ya haraka ya sekta ya Tehama ndani na nje ya nchi, hivyo miswada hii itasaidia kuondoa udukuzi, utunzaji wa taarifa, kuwalinda watoto dhidi ya matumizi yasiyofaa ya intaneti na malipo kwa njia ya mtandao,” alisema.
Alisema nia ya serikali ni kuhakikisha miswada ya sheria za matumizi salama ya mtandao inaridhiwa na wadau, inajadiliwa na kupitishwa na Bunge na kuanza kutumika, ili kuhakikisha makosa na uhalifu unaojitokeza unashughulikiwa na kudhibitiwa kikamilifu.

0 comments