Sunday, 6 April 2014

BOKO HARAM WAUA WATU 20 MSIKITINI

By    
Takribani watu 20 waliuawa jana jumamosi na kundi la Boko Haram katika msikiti wa Buni Gari ulioko karibu kilomita 105 kutoka mji mkuu wa Jimbo la Yobe kaskazini mwa Nigeria.
"Ripoti zinasema watu 20 wasio na hatia wamepoteza maisha", alisema Abdullahi Bego msemaji wa gavana wa Yobe Ibrahim Gaidam kuliambia shirika la habari la Anadolu.
Alisema wana mgambo hao wa Boko Haram waliwafyatulia risasi waislamu muda mfupi kabla ya kusaliwa sala ya Alfajiri.
"Hili ni janga. Serikali ina mamlaka ya kukomesha hili kundi licha ya jitihada zote bado wanaangamiza damu za wasio na hatia", alisema Abdullahi Bego.
Aliongeza kwa kutoa wito kwa wote walio nyuma ya mauaji haya waache kumwaga damu za wasio na hatia.
Zaidi ya watu 1,000 waliuawa katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu na kundi la Boko Haram.

0 comments