Friday, 17 July 2015

MSEMAJI WA SIMBA SC MANARA AMZUNGUMZIA BANZA STONE

By    
Oooh Rama Mate...! Nilipenda kumwita hvyo. Ni kijana wa mjini hasa. ilianza nae standard one shule ya msingi darasa moja pale Mnazi Mmoja Primary school  iliyopo mkabala na iliopozaliwa TANU (ofisi ndogo ya CCM ) New street (Lumumba) na tulikuwa sote kwa miaka miwili kabla ya wazazi kunihamishia Bunge Orimary iliopo Ohio street mkabala na ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa miaka hiyo tulikuwa na uswahiba mkubwa wa kitoto. Nikikumbuka halftime mbio zetu kwenda kwa muuza mihogo mkongwe Mzee Said na kuisukumizia na juice yake tamu ya ukwaju. 

Kipindi hcho kila tupatapo upenyo wa mapumziko, tofauti na watoto wengi wa zama zile kupenda kucheza soka. kutwa Mate alikuwa anapenda kupiga ngoma zilizokuwa ndani ya hall la shule hyo maarufu jijini. 

Sikuwa najua kuwa ndio kipaji chake. Ila kiukweli Mate alikuja kuwa mwanamuziki maarufu sana nchini na katika  moja ya tungo zake maridhawa ni wimbo wa "Mtaji wa masikini"  na ule wimbo wa "Aungurumapo simba" ambao kwa miaka mingi sasa umekuwa kama wimbo rasmi wa klabu kubwa kabisa Tanzania Simba SC. 

Mate alinizidi kidogo umri,  hvyo shule alikuwa ananikingia kifua na watoto watundu waliojaribu hata kunigusa na hakuacha kunitania tulipokuwa tukikutana enzi za ukubwani. Alikuwa haishi kunitambia kuwa yeye ni mbabe wangu na mimi  nikimwambia ilikuwa lazma unilinde kwa kuwa shule ulikuwa unaniigizia.

Kwa kweli utani ndio maongezi yaliyotawala pindi tulipokuwa tukikutana. Naandika ujumbe huu huku nikijikaza kudondosha chozi langu. Ninajua Mate...namna ulivyopigania uhai wako. Walimwengu nao hawakuacha kukuzushia kifo. Ila muumba aliamua kwa makusudi yake akuchukue leo ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kama lilivyo jina lako!

Umeacha alama Mate. Na wimbo wa "Aunguramapo Simba" naona ipo haja ya kuutukuza, hasa  hasa siku ya Simba gala mwanzoni mwa mwezi ujao. Nisiandike sana maana najijua nilivyo na uswahiba na machozi kama nilivyokuwa na uswahiba na wewe Mate. 

Kapumzike kaka 
 Inna lillah wa inna ilaihi raajiun...
Ni mimi nduguyo, rafikiyo, classmate wako
Haji Sunday Manara

0 comments