Kampuni ya uuzaji magari ya CFAO imefanya onyesho la kuonyesha bidhaa mpya walizonazo katika jengo la PSPF Golden Jubilee Tower lililopo Posta jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Modewji Blog, Meneja Masoko wa CFAO Motors, Sheikha Said amesema sababu ya kampuni hiyo kufanya onyesho katika jengo hilo ni kuwaonyesha wateja wa kampuni hiyo bidhaa mpya walizonazo katika sehemu zao wanazouzia magari (showroom).
Amebainisha kuwa, mbali na kuwaonyesha wateja lakini pia kuwaonyesha wafanyakazi na wananchi mbalimbali ambao walikuwa hawajui bidhaa zinazopatikana CFAO Motors au kwa wengine kuwa na shughuli nyingi hivyo kushindwa kufika katika 'showroom' zao na kupitia onyesho hilo wataweza kupata magari katika maeneo yao ya kazi.
“Tupo hapa kwa hili kuwasogezea huduma watu wa aina mbalimbali na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali waone bidhaa tulizonazo,” alisema Bi. Said.
Nae Afisa Mauzo wa Suzuki, David Kritsos alisema kupitia onyesho hilo wananchi na wafanyakazi wa ofisi mbalimbali wanaweza kununua magari wanayopendelea na wanaweza kusaidiwa na CFAO Motors kupata mkopo benki ili waweze kupata fedha za kununua magari hayo na kulipa mkopo taratibu.
Alisema CFAO ndiyo kampuni pekee nchini yenye nafasi ya kusambaza bidhaa za Suzuki na magari yote wanayoyauza bado ni mapya yakiwa bado hayajatumika kabisa.
Showroom hiyo itaendelea hadi hapo 4 Februari.
Moja ya Suzuki Grand Vitara magari ya CFAO yaliyopo kwenye maonyesho ya bidhaa mpya walizonazo katika jengo la PSPF Golden Jubilee Tower lililopo Posta jijini Dar es Salaam.
Moja ya Suzuki magari ya CFAO yaliyopo kwenye maonyesho ya bidhaa mpya walizonazo katika jengo la PSPF Golden Jubilee Tower lililopo Posta jijini Dar es Salaam.
Gari hilo la aina ya Suzuki linavyoonekana ubavuni..
upande wa ndani unaogawa gari hilo la Suzuki ambao unaonesha upande wa dereva na upande ambao mtu anaweza kutumia kwa kuweka mizigo na mambo mengine.
Magari hayo yanavyoonekana katika showroom hiyo ndani ya jengo la PSPF Golden Jubilee Towers.
0 comments