Tuesday, 28 May 2013

KILICHO ANDIKWA KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA 4 NA 6 KUTOKA NECTA

National Examination Council of Tanzania (N.E.C.T.A)

Matokeo ya kidato cha Sita na yale ya kidato cha nne yaliyopangwa upya yatatoka wiki ijayo kama mambo yakienda sawa. Baada ya kupangwa upya, ufaulu umeongezeka.
Kwa kutumia viwango vya zamani, matokeo mapya yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57.

Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu.

0 comments