Takribani siku 10 zimepita toka msimu wa ligi kuu ya vodacom 2012/13 toka umalizike na vilabu vikianza kuimarisha vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi unaotaraji kuanza mwezi wa nane.
Katika msimu uliopita kumeshkika kero nyingi juu ya viwanja vibovu vinavyotumika kwa ajili ya ligi hiyo. Msimu uliokwisha kati ya viwanja 10 ni vinne vilivyo kuwa na eneo zuri la kuchezea.
Msimu ujao khwanja chenye hadhi ya kutumiwa katika michezo ya kimataifa CCM Kirumba akito tumika kutokana na timu iliyokuwa unakitumia Toto Afrika kushuka daraja, lakini sina uhakika na uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo Tabora juu ya ubora wake katika eneo la kucheza baada ya kupata fursa ya michezo ya ligi kuu ya vodacom msimu ujao.
Ukiondoa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi viwanja vingine ni vile vile ukiondoa CCM Kirumba, hivyo kupelekea viwanja vyenye eneo zuri la kuchezea kusalia vitau.
Viwanja ambavyo vinasemwa kupitiliza kwenye uchakafu katika eneo la kuchezea ni Sokoine wa Mbeya ambao unataraji kutumiwa na Mbeya City na Prisons sambamba na uwanja wa Kaitaba unao tumiwa na Kagera sugar.
Vilabu vxetu vya ligi kuu ya vodacom wamekuwa na utamaduni wa kusahau ama kupuuzia katika suala ya viwanja. Vinaweza vikajitetea kuwa wao si wamiliki wa viwanja wanavyotumia na wala hawana uwezo wa kumiliki viwanja.
Vilabu vikumbuke kuwa wao nh wateja katika viwanja hivyo ndio maana kuna asilimia xa mlangoni inakwenda kwa wamiliki wa viwanja na vile vile matangazo yanayo onekana viwanjani humo, ambapo kwa namna moja ama nyingine ni sehemu ya makusanyo ya mapato kwa wamiliki wa viwanja.
Hivyo vilabu wanawajibika pia katika hili, wanauwezo wa kuwapa presha wamiliki wa viwanja katika ukarabati wa uwanja huo angalau katika eneo la kuchezea kwanza.
0 comments