Katika tembezi zangu leo nimekutana na hii post inayosema Kufuru Katika Fizikia katika kitaa cha Dinuallah,
Twenzetu kitaani kama ilivyonukuliwa
Shukrani
zote zinamstahiki Allaah Mola mlezi wa viumbe wote. Rehma na amani
zimshukie Mtume wetu na ali zake, masahaba wake na wote wenye kufuata
mwenendo wake mapaka siku ya Qiyama.
Kwa
wale waliobobea kwenye somo la fizikia wanatambua kuwa kuna kauli
maarufu inayosema “Energy can neither be created nor destroyed” katika
ile nadharia maalum ya relativity (special theory of relativity), ambapo
energy inalingwanishwa na mass katika ile formula maarufu ya E = mc2
(Energy = Mass x Speed Square), Nadharia hii imeandikwa na mwanasayansi
maarufu anayeaminiwa kuwa na akili kuliko kupindukia Albert Einstein.
Kauli
hii yenye maana "Nishati haiwezi kuumbwa wala haiwezi kuharibiwa" ni
shirki katika Rubuubiyyah ambayo ni kinyume cha Tawhid ar Rubuubiyyah.
Abapo Tawhid ar Rubuubiyyah maana yake kwa kifupi ni kumpwekesha Allaah
katika kuumba na kuviendesha (kuviendeleza au kuvipa maisha)
alivyoviumba. Hivyo kusema nishati haikuumbwa ni kosa na ni kinyume na
mafundisho wa kiislamu kwa sababu Allaah anatuambia katika Qur'aani
tukufu kwamba:
اللَّهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ
Allah ndiye Muumba wa kila kitu na yeye ndiye Mlinzi wa kila kitu (39:62)
Hivyo sisi kama waislamu hatuna budi kuamini kwamba kila kitu ikiwa ni pamoja na nishati kimeumbwa na Allaah 'azza wa jall.
Kuhusu
kwamba nishati haina mwisho kama inavyoelezewa kwenye nadharia hii kwa
vile nishati ina mzunguko usiomalizika kwa hiyo haiwezekani kuharibiwa,
Allaah anatuambia katika Qur'ani tukufu kwamba:
كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ
Kila kilioko juu yake kitatoweka. (55:26)
Siku
ambayo Allaah ta’ala atazikunja mbingu mfano wa sisi tunavyozikunja kwa
kuzizungusha karatasi mikononi mwetu, hakuna kitakachobaki. Kwa hiyo
huu ndio utakuwa mwisho wa nishati.
Hivyo
sisi kama waislamu hatuna budi kuandika kauli hii kwamba “Energy can
neither be created nor destroyed by man” yaani "Nishati haiwezi kuumbwa
wala haiwezi kuharibiwa" kwa vile mwanadamu kama nishati vyote ni viumbe
na wala hakuna mwenye uwezo wa kuumba.
Hivyo basi kuamini nadharia hii ni kufuru ambayo inaweza kumtoa anayeiamini kwenye Uislamu.
0 comments