Wednesday 26 June 2013

Adolf Hitler ; Kwanini Uingereza na Ufaransa zitabeba dhambi hii milele?

By    
Na Nova Kambota,


"Unless not later than 11 a.m , British summer time , today September
3rd ,satisfactory assurances have been given by the German government
and have reached His Majesty's Government in London, a state of war
will exist between the two countries from that hour"


Hivi ndivyo ujumbe wa serikali ya Uingereza kwenda kwa Adolf Hitler
ulivyosomeka siku ya tarehe 3 septemba 1939, masaa machache baadae
ulimwengu ukaingia katika kile kilichokuja kujulikana kama vita kuu ya
pili ya dunia (1939-1945) ambayo inaelezwa kuwa mpaka leo hii vita
hiyo imevunja rekodi ya dunia kwa kuwa vita iliyoteketeza roho za watu
wengi zaidi tangu dunia ilipoumbwa.


Tatizo kubwa ambalo wanahistoria wengi wanalifanya ni kujadili janga
hili (vita kuu ya pili ya dunia) kwa mtizamo finyu ambao mwisho wake
huwa ni kurusha lawama za upande mmoja kwa kumlaumu Adolf Hitler
pekee! Kwasababu za kitaaluma, uchambuzi na historia makala hii
inajaribu kuibua fikra mpya kwa kutanua mjadala wa nani mwenye kubeba
lawama kwa vita hii? Nifate katika makala hii ya kusisimua ambayo
itapanua uwezo wako wa kujenga hoja ……………..


Ni ngumu kueleza chimbuko la vita kuu ya pili ya dunia pasipo
kuihusisha Uingereza na Ufaransa, si sahihi kuchambua uovu wa Adolf
Hitler bila kumhusisha Chambarlain na Daladier! Kwa kutambua kabisa
Uingereza na Ufaransa "walilea" tatizo ambalo liliitumbukiza dunia
kwenye janga la vita, Adolf Hitler ni mwovu kweli ,ni mhanga wa
kihistoria , ni zao la sera dhaifu za Uingereza na Ufaransa ambazo
pasi na shaka hazina budi kugawana zigo la lawama na Ujerumani kwa
kusababisha vita kuu ya pili ya dunia 1939-1945, pasipo ubishi wowote
Uingereza na Ufaransa kwa pamoja zinapaswa kuibeba dhambi hii ya
kihistoria..........

0 comments