Wednesday 26 June 2013

HUKUMU YA KUFUNGA NUSU YA PILI YA MWEZI WA SHAABANI:

By    
Na MIMI NI MUISLAMU

Imesimuliwa na Abu Hurayra radhi za Allah ziwe juu yake.
Hakika ya mtume rehema na amani ziwe juu yake anasema:
(Itakapo ingia nusu ya shaabani msifunge) Hadithi imepokewa na Abudawd 3237.

Bila shaka hadithi hii ipo wazi kabisa katika kuharamisha kufunga nusu ya pili ya mwezi wa shaabani.Yaani kufunga kuanzia tarehe 16 ya mwezi wa shaabani na kuendelea.
Lakini kuna hadithi nyingie toka kwa mtume pia
iliyo simuliwa na Abu Hurayra radhiya Allahu anhu-amesema:
Amesema mtume rehema na amani ziwe juu yake:
(Msitangulize Ramadhani kwa kufunga siku moja wala siku mbili ,isipokuwa kwa yule aliyekuwa akifunga funga basi na afunge) Hadithi imepokelewa na Bukhari 1914.

Hadithi hii ipo wazi katika kujulisha kujuzu kufunga baada ya nusu ya pili ya mwezi wa Shaabani yaani tarehe 16 na kuendelea,kwa mtu mwenye kawaida ya kufunga funga ya siku ya jumatatu na alkhamisi,au swaumu ya kufunga siku ya kula siku. Kwani mtume kasema msitangulize ramadhani kwa kufunga siku moja na siku mbili isipokuwa kwa yule aliyekuwa akifunga basi na afunge.

Mama wa waumini Aisha radhiya Allahu anhaa anasema:
(Alikuwa mtume wa Mwenyezi Mungu-swala Allahu alayhi wasallam- akufunga mwezi wa shaabani wote,akifunga mwezi wa shaabani wote isipokuwa siku chache) Hadithi imepokelewa na Muslim 1156.
(Alikuwa akifunga mwezi wa shaabani wote.Wote isipokuwa sikku chache)
Kauli hii ya pili;{Wote isipokuwa sikku chache} yatafsiri kauli ya mwanzo.

Hadithi hii pia ipo wazi katika kujulisha kujuzu kufunga nusu ya pili ya mwezi wa Shaabani kwa yule aliyekuwa na kawaida ya kufunga hapo kabla.

Madhehebu ya Imamu Shafi wamezifanyia kazi hadithi zote hizi tatu wakasema:
Haifai kwa mtu kufunga nusu ya pili ya mwezi wa Shaabani,isipok
uwa kwa yule mwenye kawaida ya kufunga{funga za sunna kabla ya nusu ya shaabani ya pili kuingia}.



0 comments