Wednesday 19 June 2013

JE MSOMI ANAWEZA KUWA SAWA NA ASIYE SOMA?

Na Abdallah H.I Sulayman

Nikiwa kidato cha tatu pale Nur Islamic seminary iliyopo Magomeni Mapipa jijini Dar es salaam, Mama yangu alipata kuniuliza swali, sqwali ambalo lilikaa kimtego tego ambalo ni; "Je aliyesoma naweza kuwa sawa na asie soma?".

Nilitulia kwa dakika kadhaa kutafakari niipi sababu ya kuniuliza swali hilo na kumjibu hapana hawa wezi kuwa sawa. Jawabu ambalo alilikubali na kuongeza kuwa itafika mda aliye soma atakuwa sawa na asie soma.

Kauli hiyo ilinipa maswali mengi kichwani, huku swali kuu ni itakuwaje alie soma atakuwa sawa na asie soma, ambapo yalizaa maswali ulimwengu utakuwaje pale aliye soma atakuwa sawa na asie soma.

Leo nimekaa na kulitafakari upya jawabu alilo nipa mama, na kulinganisha na matukio yanayo jiri katika jamii yetu inayo tuzunguka, ambapo kuna matukio yanafanywa na wasomi na kujiuliza huyu mtu elimu yake ameipatia wapi.

Wewe uliyo kuwepo katika harakati ya kuelekea kuwa msomi unatofauti gani kati yako na asie soma katika nyanja mbalimbali.

0 comments