Thursday, 6 June 2013

TANZAGIZA KATIKA ELIMU, 7X2=15

Nilivyo kuwa shule ya msingi na y upili nilikuwa nayaamini sana majawabu yaliyomo katika vitabu, na muda mwingine nilikuwa nalazimisha jawabu lifanane na kwenye kitabu, bila kujali uwasilia wa njia nilio pita kama iko sahihi ama la.

Ni imani yangu wako wanafunzi wenye ukiritimba kama huo wa kwangu kipindi niko katika madaraja hayo ya elimu, leo katika tembezi zangu za kila siku ya magazeti nimekuta na "Serikali yaumbuka sekta ya elimu", hicho ni kichwa cha habari kilichopo katika gazeti la "Tanzania Daima".

Tuungane na Edson Kamukara tuone kilichomo kwenye hilo gazeti:

SERIKALI imeingia katika kashfa nyingine kwenye sekta ya elimu baada ya kudaiwa kuruhusu vitabu vyenye maelekezo yasiyo sahihi.

Mbunge wa kuteuliwa na rais, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) ndiye aliyeanika udhaifu uliomo kwenye vitabu vilivyoidhinishwa na serikali kutumika katika shule za msingi nchini ambapo aliviita ni sumu ya elimu.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Mbatia alionesha vitabu kadhaa bungeni huku akitaja makosa mengi yaliyomo na kuhoji viliidhinishwaje na Kamati ya Kuidhinisha Machapisho ya Kielimu (EMAC).

“Leo tunavuna tulichokipanda. Serikali imetumia fedha za chenji ya rada kusaini mikataba na kampuni zaidi ya 10 kwa ajili ya kusambaza vitabu kwenye shule zetu, lakini vitabu hivyo ni sumu kwa taifa,” alisema.

Alisema kuwa vitabu hivyo vimenunuliwa na fedha hizo sh bilioni 55.2 ambazo zilitengwa na serikali kwa ajili ya manunuzi ya vitabu na mihutasari.

Alisema kampuni hizo zilipewa mkataba wa zabuni ya kununua vitabu na mihutasari wa sh milioni 18 na ulisainiwa Machi 18 mwaka huu, huku wakitakiwa kumaliza ununuzi na usambazaji wake Septemba mwaka huu.

Mbatia alisema kuwa vitabu hivyo vikitumika vitalisababisha taifa kufa kielimu kwa vile watoto watajifunza mambo ambayo hayana ukweli.

Alitoa mfano wa kitabu cha Jiografia cha darasa la sita kilichoidhinishwa na EMAC ambacho kimekosewa kwa kuandikwa ‘Jografia’.

Vitabu vingine ni cha Hisabati cha darasa la nne katika ukarasa wa 49, ambapo imeandikwa sifuri gawanya kwa sifuri jibu lake ni sifuri wakati jibu sahihi ni haiwezekani.

Pia alisema kitabu cha Hisabati kingine kinaonesha 2x7=15 na kitabu cha Uraia pia kinaeleza kuwa ‘mtaa unaundwa na vitongoji mbalimbali na kuongozwa na wenyeviti wa vitongoji.

Mbatia alisema kitabu hicho kinasema kwamba wakazi wengi wa mtaa wameajiriwa na utumishi wa umma, viwanda na makampuni.

Alisema kampuni za Macmillan na Oxford zilizopewa jukumu la kuleta vitabu hivyo zimeshafukuzwa nchini Kenya baada ya kugundulika kuwa vitabu vyao havina ubora wa kitaaluma, lakini Tanzania imeendelea kuzikumbatia.

“Kama Rais Kikwete hivi karibuni akiwa Mbeya alikiri kuwa elimu yetu ina udhaifu, kwanini wabunge wa CCM hamtaki kukubali hili?” alihoji Mbatia na kupendekeza iundwe tume ya kudumu ya elimu itakayosimamia maslahi ya walimu, kasoro za elimu na mengineyo.

0 comments