Msikilize hapa chini akisoma taarifa yake mbele ya vyombo vya habari, hii ni moja kati ya tuhuma alizozijibu.
''Tuhuma kwamba nimekidhalilisha
chama kwa tamko la PAC kwamba Hesabu za Vyama hazijakaguliwa na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG): Katika jambo hili
ninatuhumiwa kwamba mimi kama Naibu Katibu nilipaswa kuwasiliana kwanza
na viongozi wa chama 'kuwatonya' ili wajiandae.
Kwamba kutokuwatonya
kumekidhalilisha chama na
kukiweka kundi moja na CCM na nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa
katika taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na chama chetu. Maelezo yangu
niliyoyatoa na ambayo ningependa kuyakariri hapa kuhusu jambo hili ni
kama ifuatavyo:
Utawala bora hautaki mimi kutumia nafasi yangu ya
uenyekiti wa PAC kulinda chama changu na kuonea vyama vingine. Kufanya
hivyo ni kuendeleza tabia zile zile ambazo tunazipinga na ambazo
tunapigania kuzibadilisha
Napenda kusisitiza kwamba hakuna chama
ambacho kimewahi kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali
(CAG). Natambua kwamba mahesabu ya chama changu yamekuwa yakikaguliwa na
wakaguzi wa nje kwa utaratibu tuliojiwekea. Lakini matakwa ya kisheria
ni kwamba mahesabu ya vyama vya siasa hayajakaguliwa na CAG, na hili ni
kosa la kisheria, bila kujali kosa hili ni la nani'', amesema zitto.
0 comments