Sunday, 24 November 2013

ZITTO KABWE: SIONDOKI CHADEMA NG'O

Zitto Kabwe akielezea kwa wanahabari kuwa haondoki Chadema kamwe.

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema haondoki Chadema ng'o. Adai yeye ni mwanachama halali wa chama hicho, amejiunga na Chadema akiwa na umri wa miaka 16, maisha yake yote ameyatoa kwa ajili ya kukitumikia chama hivyo hawezi kuondoka Chadema.

Ameyasema hayo muda huu wakati akiongea na wanahabari katika chumba cha mkutano kilichopo katika Hoteli ya Serena Posta jijini Dar es Salaam.

Dk. Kitila Mkumbo akiwaeleza wanahabari kuwa Zitto Kabwe hausiki na 'Waraka wa Siri'.

Naye Dk. Kitila Mkumbo aliyevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu Chadema amekubali kuwa 'Waraka wa Siri' uliosomwa kwa wanahabari na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu juzi na kusababisha kuwavua vyeo Zitto Kabwe, yeye na Samson Mwigamba ni yeye aliyeuandaa lakini Zitto Kabwe hausiki kabisa.

Wakili wa Zitto Kabwe, Albert Msando ametaja maswali kadhaa ambayo yanahitaji kujibiwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu yakiwemo:

Wakili wa Zitto Kabwe, Albert Msando akitaja maswali mabayo yanahitaji majibu kutoka kwa Tundu Lissu.

-Utaratibu gani uliotumika kuwavua vyeo akina Zitto Kabwe?
-Ushahidi gani alionao au alioutumia kumvua vyeo Zitto Kabwe na wenzake?
-Sababu gani za kumhusisha Zitto Kabwe katika mkakati wa siri wakati Dk. Kitila amesema hausiki?
-Utaratibu gani utatumika kuwaandalia mashitaka?

0 comments