Tuesday, 26 November 2013

ANGOLA YAIPIGA MARUFUKU DINI YA KIISLAMU:

(Hakika wale walio kufuru hutoa mali zao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watazitoa mali hizo, kisha zitakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam) Qur ani 8:36

Vita kati ya haki na batili ni vita ya muda mrefu,
na itaendelea mpaka pale Allah atakapoirithi ardhi hii na vilivyomo.

Makafiri wamekuwa wakitumia mbinu mbali mbali
ili kupambana na uislamu dini pekee ya Allah.
Wamejisahau ya kwamba
kwa vitendo vyao hivyo,wanapigana vita na Mwenyezi
Mungu,ni nani atakaye mshinda Allah muweza wa kila jambo
Muumba wa ulimwengu na vilivyomo,mjuzi wa kila kitu???

Katika vita vyao dhidi ya uislamu,makafiri wametumia
njia mbali mbali,miongoni mwa njia hizo ni kuwaadhibu waislamu watu wa haki.Nayo angola yatangaza kupiga marufuku uislamu nchini humo.

Kana kwamba njia hiyo wameona haitoshi na wakaona waongeze njia nyingine nayo ni njia ya kushambulia
vile vitu vitukufu kwa waislamu.
Wamemkashifu mtume wetu Muhamadi rehema
na amani ziwe juu yake,na wameamua kujaribu kuchafua
kitabu chetu kitukuf cha Qur ani.
Bila shaka matukio haya yanaashiria hali mbili:
1)Kuenea kwa kasi kwa uislamu.
2)Udhaifu wa waislamu.

Makafiri wameghadhabishwa na kuenea kwa kasi
kwa uislamu, mpaka katika ngome zao.Wao wenyewe wamekiri na kusema uislamu ni The fastest Growing Religion: yaani Uislamu ni dini inayokuwa kwa kasi.Kutokana na hivyo wameamua kuzidisha juhudi zao katika kupambana na uislamu.
Nasi tunawambia uislamu ni dini ya Allah hakuna atakaye weza kupambana nayo. Kufeni kutokana na ghadhabu zenu.Mtatoa kila kitu kwa ajili ya kupambana na uislamu,kisha mtashidwa.
Allah anatueleza ndani ya kitabu chake kitukufu:
(Hakika wale walio kufuru hutoa mali zao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watazitoa mali hizo, kisha zitakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam) Qur ani 8:36

Tunawaambia Vita vyenu dhidi ya uislamu haviongezi isipokuwa kuzidi kuwazindua waislamu walio lala,vile vile kuulingania uislamu kwa ndugu zenu wasio kuwa waislamu,kwani pindi wanaposikia na kuona vita hivi dhidi ya uislamu hutaka kujua uislamu ni nini na hatimaye kuufuata ukweli.
Kuna vijana wawili wa kimarekani marafiki waliwafiqishwa kuelekea hija. Moja ya mashekhe pindi alipo kutana nao aliwauliza,
Je nyinyi mmezaliwa waislamu au mmesilimu?
Wakajibu tumesilimu.
Akawauliza ni nani aliye kusilimisheni /au aliye kuwa ni sababu juu yenu kusilimu?
Wakajibu :Bushi ndiye aliye tusilimisha.
Akashangaa na kuuliza:Kivipi?!
Wakajibu:Wanasema sisi tulikuwa hatuujui uislamu hata kidogo,neno lenyewe uislamu tulikuwa hatujawahi kulisikia !
Baada ya bushi kutanganza vita dhidi ya uislamu katika matukio ya September 11,tukaulizana kati yetu hivi uislamu ni nini?
Tukaingia internet na kutafuta maana ya neno Uislamu.
Tukagundua kumbe ni dini na ikatufurahisha,tukaona huu ndio mfumo wa maisha unao takiwa kufutwa,hatimaye tukasilimu.

Vile vile ni juu yetu kukubali ya kwamba udhaifu wetu
ni miongoni mwa sababu zilizo pelekea hali hii.Kwani iwapo waislamu tunanguvu,basi makafiri hawato thubutu kufanya vitendo kama hivi.Ni juu yetu kurudisha ukakamavu wetu,
kurudisha miongoni mwetu mfano wa akina Anasi bin Nadhwir,Khalidi bin Al waliid,Abuu Ubaida Aamiir bin Al jaraah,Aliy bin Abii Twaalib
na wengineo wengi.
Kama anavyo waelezea Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Qur ani:
(Miongoni mwa Waumini kuna wanaume {vidume} walio timiza waliyo muahidi Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha {ahadi} hata kidogo) Qur ani 33:23

Je wewe ni miongoni mwa watu walio muwekea ahadi
Mwenyezi Mungu juu ya kuufuata uislamu na kuutetea
kwa lolote lile ???

0 comments