Bunge la Uganda limepitisha muswada unaopiga marufuku wanawake kuvaa
sketi fupi, pamoja na vitendo vinavyochochea ngono, limeripoti gazeti
binafsi la Daily Monitor.
Muswada huo uliopendekezwa mwaka 2011 unapiga marufuku pia video za ngono, miziki na hata ngoma zinazochochea vitendo hivyo.
Serikali ya Uganda inasema kuwa, picha za ngono zimekuwa tatizo kubwa
kwa jamii na huchochea jinai za ngono dhidi ya wanawake na watoto kama
vile kubakwa na kutumiwa watoto wadogo katika ngono.
Kwa
mujibu wa sheria hiyo mpya ni marufuku kuacha wazi baadhi ya sehemu za
mwili kama vile makalio, mapaja na matiti na kutenda kitendo chochote
kinachochoea hisia za ngono.
Chanzo: ahbaabur
0 comments