
BAADA ya kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Yahaya’, mwanadada anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongo fleva, Judith Wambura ‘Jide’ amesambaza kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Historia’.
Kwa mujibu wa mitandano ya kijamii, wimbo huo umesambazwa hivi karibuni na tayari umeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio, kutokana na umakini wa mwanadada huyo.
Jide, alisema katika wimbo huo amesimulia baadhi ya maisha yake ikiwa ni pamoja na historia za maisha ya watu wengine, na kwamba una mafunzo kwa jamii nzima bila kubagua rika.
“Nina imani kazi hii itafanya vizuri, kwani tayari nimeisambaza na nimeona mapokezi yake, naomba sapoti kwa wapenzi wa kazi zangu, nipo katika mchakato wa kuanza kupiga picha za video kwa ajili ya wimbo huo,” alisema.
Jide alishawahi kutamba na kazi zake kama, ‘Malaika’, ‘Joto Hasira’ na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
0 comments