Na Mbarak Said kutoka katika kitaa cha ISLAMIC CENTRE FOR RESEARCH (ICR)
Nimelelewa katika jamii ambayo sherehe za maulidi ni kama ada kwao, nimehudhuria na kushirki kusoma.
Baada ya miaka kupita nami kufungua macho nimekuwa nikiangalia sherehe
za maulidi katika fikra nyengine, yawezekana isiwe sawa, lkn ndio fikra
nilionayo na kila mtu ana uhuru wa kuwa na fikra zake.
Huwa nawaza na hujaribu kuwafikishia wengine fikra hii
Hivi tunaonaje iwapo tutayatumia maulidi kama FURSA ya kuyatatua baadhi ya matatizo katika jamii yetu.
Kwa mfano.
Badala ya kuchangishana mamilioni ya fedha kwa kuhudumia hadhara hizi
kwa vyakula na mengineyo, kwanini tusijiwekee mpango mbadala kwamba,
kila mwaka tutachangisha fedha na fedha hizo zitatumika kujenga madrasa
na mashule na hata kuimarisha misikiti. Yaani twaweza tumia fedha na
watu kujitolea nguvu kazi kwa kuadhimisha mazazi ya mtume.
Kiasha tunajiwekea malengo malengo, na kila maulidi yanapofika
tunaangalia malengo yetu tumefikia wapi maulidi ya mwaka uliopita na ya
mwaka tujiwekea malengo yepi. Kisha tunaelezana kwamba tumeweza kujenga
madrasa kadhaa, au tumefanya matengenezo kadhaa, au tumenunua vitabu
kadhaaa kwa ajili ya mashule au madrasa, au tumejenga zahanati ama
hospitali hii ama ile, na kwa mwaka ujao tunajiwekea malengo haya ama
yale.
Naamini kwa kufanya hivyo tutakuwa hatujapoteza lengo la maulidi na yawezekana ikawa tumepiga ndege wawili kwa jiwe moja.
Hebu angalia maadhimisho kama ya mapinduzi, kila mwaka huwa wanasema tumejenga kadhaa na tumefanya kadhaa.
Nasema ni FURSA kwa vile wengi wetu huwa tayari kujitolea kwenye maulidi kwa hali yoyote tulionayo, nimeshuhudia hayo.
Unakuta gharama ya maulidi ni kubwa, lkn angalia msikiti wa hao
waliotoa fedha ulivyo, angalia madrasa nk. Ziko hali ileile au mbaya
zaidi ya maulidi iliyopita.
IELEWEKE, SIKATAZI KUSOMWA MAULIDI,
........najua kuna wataosema , aaa wapinga maulidi wana hoja nyingi za kulazimisha kuyazima maulidi. ........
Laaaa hapana sio lengo langu hilo, bali lengo langu ni kutoa fikra tu ili iwapo itawezekana tubadili mwelekeo na tutumie FURSA.
HIYO NI FIKRA YANGU
0 comments