Shahnaz
Laghari ni mwanamke wa kiislamu anayevaa 'baparda' ameweka rekodi na
kuingia katika kitabu cha Guiness (Guiness book of world record) kwa
kuwa mwanamke wa kwanza duniani wa namna hiyo kuendesha ndege.
Baparda
ni aina ya Baibui pana pamoja na Niqabu linakaribiana na Burqa. Shahnaz
Laghari ameonesha uwezo wa kurusha ndege peke huku akiwa katika mavazi
kamilifu ya stara ya kiislamu.
Shahnaz ambaye mwaka
2013 aliwania ubunge kama mgombea binafsi ameonesha kwamba mtu anaweza
kufanya jambo kubwa la kimaendeleo na bado akaendelea kubaki katika
mipaka ya dini.
Rubani huyo ni mtetezi mkuu wa haki za wanawake wa Pakistan. Aidha
anajitolea kuwasaidia wanawake wa kwa kufungua vituo vya elimu ya bure
na vituo vya kushona kwa ajili ya wanawake maskini katika Pakistan.
akijiandaa kushuka katika ndege |
![]() |
Baada ya kushuka |
![]() |
Akirusha ndege |
Ndani ya ndege |
![]() |
Katika harakati za kuwasaidia wanawake wenzake |
CREDIT: Ahbaabur Rasuul
0 comments