![]() |
polisi wakiwa ndani ya msikiti na viatu |
![]() |
walitanda mitaa yote |
![]() |
waislamu wakimsaidia mwenzao aliyejeruhiwa |
![]() |
majeruhi |
![]() |
kipigo kwanza ,halafu panda karandinga |
![]() |
wakipandishwa katika karandinga |
![]() |
majeruhi |
Watu wawili wanaarifiwa kuwa wameuawa na wengine kadha kujeruhiwa kwenye ghasia katika Masjid Mussa ulioko majengo mjini Mombasa, Kenya.
Polisi walivamia msikiti huo baada ya kupata taarifa kuwa
kuna kundi la vijana lilikuwa likiendesha mafunzo ya kijeshi msikitini hapo.
Hatua hiyo ya polisi iliibua ghasia ndani ya msikiti huo wa Masjid Mussa uliopo katika maeneo ya Majengo na katika mitaa ya jirani. Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na kumekuwepo na taarifa kuwa risasi za moto zilitumika kuudhibiti umati wa watu waliokuwa wakiwarushia mawe polisi.
Kijana mmoja na Askari polisi mmoja wameripotiwa kufa.
Kamanda wa Polisi mkoa Mombasa Robert Kitur alisema askari huyo alikufa baada ya kupata majeraha makubwa usoni.
Aidha alisema askari mwingine alikimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu ya tumbo. Polisi walitumia mabomu ya machozi, risasi za raba na za moto katika kukabiliana na waislamu hao.
Zaidi ya vijana mia moja wamekamatwa. Hata hivyo, maelezo ya mkuu huyo wa polisi hayajathibitishwa na vyanzo huru.
Mwezi Agosti 2012 watu waliojifunika nyuso walimuua kwa kumpiga risasi Imamu wa Msikiti huo, Sheikh Aboud Rogo, aliyekuwa akitoa mahubiri hapo na ambaye serikali za Marekani na Kenya zilikuwa zikimshutumu kutoa mafunzo na kufadhiliwa na kundi la Al Shabab la Somalia lenye
mafungamano na wapiganaji wa Al Qaeda.
Mwaka mmoja baadaye, mrithi wa sheikh Rogo, Sheikh Ibrahim Rogo aliuawa katika shambulizi kama hilo. Matukio yote mawili yaliibua ghasia katika mji huo.
Waislamu nchini Kenya wanawatuhumu wanausalama kuhusika na vifo hivyo, shutuma ambazo polisi wamekuwa wakizikanusha.
![]() |
baadhi ya waliokamatwa |
![]() |
wakiwa chini ya ulinzi |
![]() |
takbiir Allah Akbar |
0 comments