Mwandishi Wetu, DODOMA
Wasichana
wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali mjini hapa
wameelezea neema iliyowafikia kufuatia kujikusanyia pesa ndefu kutoka
kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba ambao wanadaiwa kuwalipa
vizuri.
Wakizungumza
na Ijumaa kwa nyakati tofauti, wadada hao ambao baadhi wanatokea Mikoa
ya Dar, Arusha, Mbeya na kwingineko walisema kipindi hiki wanakiita ni
cha mavuno kwao kwani waheshimiwa hao si watu wa kulipa pesa ndogo
wanapowaopoa.
“Yaani
sasa hivi ni kipindi cha mavuno, wateja ni wengi na wanalipa vizuri
tofauti na kipindi cha nyuma. Kwa mfano ukibahatika kumpata mjumbe wa
bunge hili linaloendelea sasa, mbona utafurahi na roho yako! Wanalipa
vizuri ile mbaya.
“Kipindi
cha nyuma unaweza kulala na mtu akakulipa shilingi 30,000 au 20,000
lakini sasa hivi ni 50,000 kwenda juu, hakuna longolongo, tusipojenga
safari hii basi tena,” alisema msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina
la Husna ambaye kiwanja chake kikuu cha biashara ni eneo Chako ni
Chako.
Mwingine
ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini akidai yuko Dodoma bila
ndugu zake walioko Dar kujua alisema: “Unajua hii biashara inakuwaga na
usumbufu sana, unaweza kuchukuliwa na mtu asikulipe lakini sasa hivi
wateja wetu wakuu ni hawa wabunge, wengine wametugeuza nyumba ndogo zao
kabisa.”
Hata
hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, biashara hiyo sasa
imeshika kasi kiasi kwamba baadhi ya waheshimiwa humalizia posho zao za
siku kwa kuzitumbua na madadapoa hao.
Mwandishi
wetu alifanya doria siku za wikiendi maeneo ya Chako ni Chako, Mwenga
Bar na zaidi katika kumbi za starehe kama vile Club 84 na Maisha na
kushuhudia magari yakipaki na kupakiza wasichana kisha kuondoka.
Gazeti
hili linatumia nafasi hii kuwaasa waheshimiwa kufanya walichokifuata
bungeni na kuacha michepuko isiyokuwa na maana na wale wasichana
walioona njia sahihi ya kutafuta maisha bora ni kwa kujiuza, wajue
kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.
0 comments