Viongozi wa nane wa taasisi na mashirika makubwa ya kiislamu nchini Marekani wametangaza kuzindua Baraza la waislamu litakalokuwa linayaunganisha taasisi zote hizo zilizokubaliana kushirikiana.
Katibu mkuu mpya wa baraza hilo la taasisi/mashirika ya kiislamu, U.S. Council of Muslim Organizations (USCMO) Oussama Jammal alisema kwamba jambo hilo limekuwa likisubiriwa kwa muda mrefu na waislamu wa marekani.
Alisema kuwa wamefurahi taasisi zote kubwa zimekuwa pamoja katika kukabiliana na matarajio na matumaini ya waislamu wa kaskazini mwa marekani.
Taasisi na mashirika ya kiislamu yanayounda baraza hilo ni, American Muslims for Palestine, Council on American-Islamic Relations (CAIR) na Islamic Circle of North America.
Nyengine ni Muslim American Society,Muslim Legal Fund of America, Muslim Alliance in North America, Muslim Ummah of North America, na The Mosque Cares.
Kwa mujibu wa Jammal, USCMO lengo lake la kwanza ni kufanya sensa ya waislamu wa Marekani na pia kuongeza ushiriki wa waislamu katika siasa za Marekani hususani katika Uchaguzi ujao.
Kufikiwa kuundwa kwa baraza hilo kumekuchukuwa zaidi ya miaka miwili kwa matumaini ya kuwasaidia waislamu kuwa pamoja na kuweza kuwasiliana kwa karibu na kutengeneza uislamu ulio bora kwa wamarekani.
CHANZO: AHBAABUR RASUL

0 comments