Kampuni kubwa zaidi ya vinywaji duniani Coca-Cola,
inapanga kuondoa kiungo tatanishi katika baadhi ya vinywaji vyake
ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Hii ni kufuatia shinikizo kutoka kwa wateja wa
vinywaji hivyo nchini Marekani waliotia saini ujumbe wa kusihinikiza
kampuni hio kuondoa kiungo hicho kupitia kwenye matandao. Kiungo hicho ni kemikali yenye mafuta ya kupikia iitwayo (Brominated vegetable oil au BVO) inayopatikana katika vinywaji kama Fanta na Powerade kinywaji cha kuongeza mwili nguvu.
Kampuni hasimu ya vinywaji Pepsi iliondoa viungo hivyo vya kemikali kutoka katika kinywaji chake kijulikanacho kama Gatorade mwaka jana.
Nchini Japan na katika muungano wa Ulaya kiungo cha BVO hakiruhusiwi kuongezwa katika vyakula au vinywaji.
Je nini umuhimu wa kiungo cha BVO?
Kampuni ya Coke hukitumia ili kuzuia viungo vingine vilivyo katika vinywaji hivyo kuachana.
Lakini watafiti wanasema kuwa kiungo hicho kinaweza kusababisha mtu kuwa msahaulifu ,kupata maradhi ya ngozi na matatizo ya Neva za mwili.
Hata hivyo msemaji wa kampuni ya Coke Josh Gold amesema kuwa hatua ya kuondoa kiung hicho sio kutokana na tisho la kiafya kwani vinywaji vyake vyenye kiungo cha BVO viko salama na daima vimekuwa salama.
Kampuni hiyo imesema kuwa kiungo cha BVO hakitumiki sana katika nchi nyingi lakini kitaondolewa katika bidhaa zake zinazouzwa nchini Canada na Marekani ya Kusini.
Hatua ya Coke imetokana na shinikizo za watu na wadadisi wanasema kuwa ni funzo kwa kampuni nyingine kuanza kuhakikisha usalama wa bidhaa za o kiafya.
Kampeini hiyo ilianzishwa na kijana mmoja anayeishi katika jimbo la Mississippi, aliyehoji kwa nini Coke inatyumia kiungo hicho katika vinywaji vinavyotumiwa na wanariadha.
CHANZO: BBC SWAHILI
0 comments