Monday, 19 May 2014

SUDAN KUSINI WAPOKEA MKONO TOKA KWA MSUMBIJI

Jitihada za mara ya kwanza kwa Sudan Kusini kufuzu kucheza mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika zimekatishwa tamaa na kipigo cha magoli 5-0 kutoka kwa Msumbiji, katika mechi ya duru ya kwanza.

Goli la kwanza lilifungwa na Josimar Machaisse. aliyefunga kutoka nchani mwa 18 alipounganisha krosi iliyoingia kutoka upande wa kushoto.

Dakika nne kabla ya mapumziko, mlinzi Mexer aliachiwa nafasi nje ya eneo la hatari kisha akakung’uta mkwaju wa juu uliotikisa pembe ya nyavu.

Magoli mengine matatu yalitoka kwa Sonito na Isac Carvalho.

Matokeo ya mechi nyingine ni kama ifuatavyo:-
Madagascar 2 – 1 Uganda 
Kenya 1 – 0 Visiwa vya Comoro 
Liberia 1 – 0 Lesotho 
Swaziland 1 -  1  Sierra Leone 
Burundi 1 –  1 Botswana
Central African Republic 0 – 0 Guinea Bissau 
Libya 0 – 0  Rwanda

0 comments