Thursday, 3 July 2014

WAKAZI WA MOROGOROGO WAKO HATARINI, KUTOKANA NA MINARA

Wakazi wa mkoa wa Morogoro wako hatarini kukumbwa na athari zinazotokana na mionzi ya minara ambayo mingi imekuwa ikijengwa kwa kasi karibu na makazi ya watu katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Athari hii inatokana na uendeshwaji wa miradi mingi mkoani humo na nchini hasa ujenzi wa minara ya simu zaidi ya elfu 15 unaofanyika bila kufanywa tathmini ya athari za kimazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.

Miradi ya minara mingi hivi sasa mkoani Morogoro inajengwa kwenye makazi ya watu.

Watalaamu wanasema mionzi ya minara hii ni hatari kwa afya ya wananchi.

Sheria ya Mazingira sura ya 191 ya mwaka 2004 inataka shughuli zote za maendeleo zifanyiwe tathmini ya mazingira ili kubaini athari zinazoweza kusababishwa na shughuli hizo na kuzitafutia ufumbuzi. Je hili linafanyika .

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeona hili na kuendesha mafunzo ya tathmini ya mazingira kwa maafisa mazingira kwa kuanzia kanda ya kaskazini wakati maagizo yakitolewa.

Baadhi ya wananchi mjini Morogoro wamesema hawana uelewa juu ya athari za minara karibu na makazi yao.

Washiriki wa mafunzo hayo ni maafisa kanda na wataalamu ngazi za wilaya kutoka mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

0 comments