Bingwa wa mchezo wa tenisi kwa upande wa akina dada duniani Serena Williams amekosoa matamshi aliyoyataja kuwa ya kibaguzi na kutojali ujinsia yaliotolewa na rais wa shirikisho la Tenisi nchini Urusi Shamil Tarpischev dhidi yake na dadaake Venus Williams.
Katika mazungumzo yake Tarpischev aliwaita kina dada hao wawili kama ''kaka wawili'' .
Hatahivyo afisa huyo alipigwa faini ya pauni 15,500 na kupigwa marufuku ya mwaka moja kwa kutoa matamshi hayo aliyoyataja kama ya mzaha.
''Sikuyapendelea hata kidogona nadhani watu wengi pia hawakuyapendelea''.
matamshi ya Bwana Tarpischev pia yalishtumiwa na shirikisho la mchezo wa Tenisi duniani WTA pamoja na shikisho la mchezo huo nchini marekani USTA.
CHANZO: BBC SWAHILI
0 comments