Sitti ameingia katika mzozo na mamlaka za Serikali baada ya kudaiwa kukiuka kanuni za uendeshaji wa mashindano hayo kwa kuwasilisha cheti kinachoonesha umri ulio kinyume cha umri wake halali, jambo ambalo kwa mujibu wa taratibu za mashindano hayo, hakupaswa kushiriki.
Mshindi huyo wa kitongoji cha Chang’ombe na kisha Kanda ya Temeke, anadaiwa kughushi cheti kipya cha kuzaliwa kilichotolewa Septemba mwaka huu kinachoonesha kuwa alizaliwa mwaka 1991, badala ya kile cha awali ambacho kinaoonesha alizaliwa Mei 31, 1989, umri wake sahihi unaomfanya awe na miaka 25.
Kwa mujibu wa taratibu za Kamati ya Miss Tanzania, warembo wanaoshiriki shindano hilo hawapaswi kuzidi umri wa miaka 23, umri ambao tayari kwa mujibu wa vielelezo kadhaa umevukwa na Sitti.
Akizungumza jana kwa simu na gazeti hili, Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Lebejo alisema wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo na kwamba wiki hii watakutana na Lundenga.
Wakati Basata ikieleza hayo, habari zinadai kuwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), wamekwisha kukifuta cheti kinachotangazwa kupatiwa Sitti, Septemba mwaka huu, kwani si halali kwa mujibu wa vielelezo vyao.
Inadaiwa kuwa Rita baada ya kufikia uamuzi huo, imeiarifu Basata ikiitaka ichukue hatua stahiki kwa mrembo huyo ikiwamo kumvua taji hilo, lakini Lebejo alisema jana kuwa wao kama hilo lipo hivyo ni la Rita, kwa sababu wao hawashughuliki na vyeti, bali wakala hao
CHANZO: HABARI LEO
0 comments