Tuesday, 4 November 2014

SERIKALI YAITAKA MAMLAKA YA MAJI KUWACHUKULIA HATUA WAFANYAKAZI WAKE

By    
Serikali imeziagiza mamlaka za maji na usafi wa mazingira nchini, kuhakikisha zinachukua hatua dhidi ya baadhi ya wafanyakazi wao, wanaotajwa kuwa chanzo cha kuwepo kwa uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali nchini.

Agizo hilo limetolewa mjini Dodoma na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa mamlaka za maji mijini, na kusisitiza kuwa upotevu wa maji unachangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya wafanyakazi kuhujumu miundombinu hiyo kwa lengo la kujinufaisha huku wakisingizia uchakavu wa mabomba.
Pamoja na mambo mengine, Profesa Maghembe amezitahadharisha mamlaka hizo za maji, kuhakikisha zinakopa kwa weledi katika benki mbalimbali, ili madeni hayo yawe stahimilivu na kuziwezesha mamlaka hizo kujiendesha kwa tija

0 comments