Monday, 13 July 2015

NEC YATANGAZA MAJIMBO MAPYA 26 YA UCHAGUZI

By    
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya uchaguzi ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kukata kwa majimbo hayo wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia  katika majimbo mapya.

Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.

Majimbo yaliongezwa ni Handeni Mjini, Nanyamba, Makambako, Butiama, Tarime Mjini, Tunduma, Msimbo, Kavu, Geita Mjini, Mafinga Mjini, Ushetu, Nzega Mjini, Kahama Mjini, Kondoa Mjini, Newala Mjini, Bunda Mjini, Mbulu Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini, Mbagala, Kibamba,Vwawa,Monongo,Mlimba, Pamoja na Uliambulu.

Jaji Lubuva amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika Halmashauri mbili hiyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki katika Halmashauri moja tu.

Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.

Chanzo: www.issamichuzi.blogspot.com

0 comments