Sunday, 9 August 2015

AN-NAHl WAWAPONGEZA WALIOFANYA VYEMA KIDATO CHA SITA

Taasisi ya An-nahl Trust leo imewapongeza wahitimu wa kidato cha sita waliofanya vyema katika mitiano yao ya kidato cha sita wa mwaka huu (2015), ambapo matokeo yao yalitoka mwezi uliopita.

Katika hafla hiyo ya kuwapongeza kulizungumzwa mada mbalimbali ya namna wanavyo weza kufikia malengo yao walio jiwekea, na utoaji wa zawadi zilizo andaliwa kwa ajili yao.

Katka hafla hiyo iliyoanza mida ya saam bili mapa saa saba mchana iliuzuriwa na muhitimu aliyeongoza wahitimu wenzake wote kitaifa, ndugu Ramadhan Gembe kutoka Fedha Boy na aliye waongoza wasichana toka Fedha girl.

Ramadhan Gembe akiongea mara baada ya kupokea zawadi yake ya Laptop na vitabu vya Dini
Gembe alisema kuwa anawashukuru wazazi wake wote kwa mchango alioupata kutoka kwao, na kuwataka vijana wenzake kushikamana na dini ili waweze kupambana vyema na changamoto za maisha.
Ramadhan Gembe akipokea zawadi yake kutoka kwa mkurugenzi wa Al-maktoum Foundation Tanzania na principle wa Al-maktoum college of Engenieering and Technology, Dr. Hamdun I. Sulayman
Mgeni Rasmi wa Hafla hiyo, Dr. Hamdun Ibrahim Sulayman akitoa kalima
Amir wa An-nahl, Engineer Ally Kilima akitoa mada ya time managment
Amir wa An-nahl akiwahimiza waliopekea zawadi ya vitabu kwenda kuvisoma, si kuvifungua kwenye makabiti, akitolea mfano wa kijana aliyezawadiwa kitabu ndani yake akawekewa Checki ya Banki, na kwa kuto kukisoma kitabu hicho, kulimpelekea kuzikosa fedha hizo
Mwanadada aliyewaongoza wanawake wenzake kuutoka Fedha Girl akipokea zawadi toka kwa viongozi wa An-nahl kina mama.
















0 comments