Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa pamoja na kutolea ufafanuzi malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yenye lengo la kufuta kabisa umaskini.(Picha zote ne Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa yatakayofanyika siku ya Jumanne Tarehe 13, Oktoba katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez.
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiendelea kufuatilia yanayojiri kwenye mkutanoni na waandishi wa habari.
Waandishi wa habari wakifuatilia kinachoendelea mkutanoni.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakiwa wameshikilia lengo namba 1 na 13 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Agha Khan, Iman Kawambwa akiwa ameshikilia lengo namba 4 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wameshikilia lengo namba 5 na 10 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akiwa ameshikilia lengo namba 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Afisa Habari wa Shirika la kazi duniani (ILO) Tanzania, Magnus Minja na Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo wakiwakilisha lengo namba 1 na 8.
Baadhi ya wandishi wa habari wakiwa wameshika namba mbalimbali za malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Na Mwandishi wetu
Kila Oktoba 24 ya kila mwaka, Umoja wa Mataifa huadhimisha siku ya kuundwa kwake. Kwa mwaka huu Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yanayofanya kazi kama taasisi moja yameendelea kujishughulisha na kazi mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuadhimisha miaka 70 ya kuundwa kwa umoja huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez kuhusu umuhimu wa malengo hayo amesema "Kwa hakika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ni wito wa kujitazama, kuona yale tuliyofanya kwa miongo kadhaa na kujikita kuona namna ya kuabiliana na umaskini hapa nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla
"Malengo ya Maendeleo endelevu ni wito wa kuwajibika kwetu sote. Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa akiwa peke yake. Inabidi tufanye kazi kwa pamoja,wadau wote,serikali na bunge, vyama vya kiraia, madhehebu ya kidini, wafanya biashara, wajasiliamali, na wanazuoni.Na hakika tukishirikiana kwa nguvu pamoja na amani tunaweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu"
Pia alisistiza kuwa “Malengo ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya.
Zimelenga kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
Akizungumzana waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya amesema kuwa nia ya serikali ni kuendelea kushirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa na kuwatakawatengeneze sera nzuri ambazio zitahakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma katika mipango ya maendeleo ya kitaifa.
Aliendelea kufafanua kwa kusema Tanzania inafurahishwa na ukweli unaoonekana kwenye malengo mapya ya maendeleo endelevu kwani yamechota pia yale malengo ya milenia ambayo yalikuwa bado hayajamaliziwa kwani katika hayo kunaweza kuleta mabadiliko ya kuwezesha kuondokanana umaskini katika sura zake zote ifikapo mwaka 2030.
Maadhimisho ya Umoja wa mataifa yatafavyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne Oktoba 13 badala ya siku iliyozoelekaya Oktoba 24 ili kupisha uchaguzi mkuu wa Tanzania unaofanyika Oktoba 25. Na kauli mbiu ya maadhimisho ya Umoja wa mataifa mwaka huu ni "Umoja wa Mataifa uliothabiti, Dunia bora".
0 comments