Rooney anashikilia rikodi ya kugunga magoli ambayo yaliiwezesha Manchester United kuibuka na ushindi ambapo amefunga jumla ya magoli 29, akifuatiwa kwa karibu na kocha msaidizi wa kikosi hicho Ryan Giggs ambayeamefunga magoli 27.
Rikodi hiyo ameweza kuifikisha baada ya kuiwezesha United kuibuka na ushindi mbele ya Liverpool na Sheffiel United katika michezo iliyochezwa mapema mwaka huu.
Katika magoli hayo 29 ya kuamua ushindi kwa united Rooney amefunga magoli 16 katika ushindi wa goli 1-0, ambapo kwa mara ya kwanza alifanya hivyo katika mchezo dhidi ya Livepool mwaka 2005 uliochezwa katika uwanja wa Anfield.
Anaemfuata kwa karibu katika kuiwezesha Man U kuibuka na ushindi wa goli 1-0 ni Eric Cantona, Mark Hughes na Brian McClair kila mmoja akifanikiwa mara 12, wakati Ryan Giggs na Lou Macari wao wakiwa wamefanya hivyo mara 11.
0 comments