Tuesday, 12 January 2016

KATIBU MWENEZI CCM MKOA WA MWANZA ATOA MAAGIZO KWA WAWAKILISHI WA WANANCHI.

By    
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangellepa akiongea na Wanahabari katika ofisi za Chama hicho Mkoa wa Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, kimewataka viongozi mbalimbali Mkoani Mwanza, kuwatumikia vema wananchi waliochagua na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Simon Mangellepa mbele ya wanahabari, wakati akitoa shukrani kwa makundi mbalimbali ya wananchi ambayo ni pamoja na machinga, wakulima, wavuvi pamoja na wafanyabiashara kwa namna walivyojitoka kwa hali na mali kukisaidia chama hicho kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Mangellepa amesema kuwa uchaguzi umemalizika hivyo ni vema viongozi wote ambao ni pamoja na Mabalozi, Wenyeviti wa Serikali za Mtaa na Vijiji, Madiwani pamoja na Wabunge wakaacha kuwatumikia wananchi kwa mazoea na badala yake wawakilishe vizuri katika ngazi za maamuzi katika kutatua matatizo yao.

“Hii kauli ya Hapa Kazi Tu haishii kwa Magufuli peke yake (Rais John Pombe Magufuli), mimi nasema inaanzia hata kwa mabalozi, wenyeviti wa vitongoji, mitaa, madiwani na wabunge. Chama cha Mapinduzi Mkoa kinawataka Madiwani na Wabunge warudi kwa wananchi ili wanapokwenda kuwawakilisha wananchi wawakilishe mawazo sahihi ya wananchi wao”. Alisema Mangellepa.

Kauli ya Chama hicho imeungwa mkono na baadhi ya wananchi Jijini Mwanza ambao wamewakumbusha viongozi wao kuhakikisha kwamba wanatatua changamoto zinazowakabili ambazo ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana, ubovu wa miundombinu, kushughulikia kero ya upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma za afya katika ngazi za Kata ili kutimiza ahadi walizozitoa wakati wa kampeni zao.
Bonyeza PLAY Hapa Chini Kusikiliza

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangellepa akiongea na Wanahabari katika ofisi za Chama hicho Mkoa wa Mwanza.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangellepa akiongea na Wanahabari katika ofisi za Chama hicho Mkoa wa Mwanza.
Wanahabari

0 comments