Friday, 15 January 2016

KUTOKA FB: WASOMI WA KISASA

‪#‎WasomiWaKisasa‬
Na bado atatokea mtu akuulize, 'Yaani Msomi mzima halafu una....'
Bado kuna watu huamini kuwa Wasomi watakuja kuikomboa nchi.
Well, wamekuwepo tangu enzi za Nyerere, wameendelea kupokea mishahara (mikubwa na midogo), wamepatia humo mitaji ya kuanzisha biashara bila stress huku wakitumia kazi ya Serikali kama bima yao, wameendelea kudai kuajiriwa licha ya kuwa wameelimika kuliko wasiosoma na wakiwa vyuoni wamefanywa kuwa Tabaka la peke yao, wakitetewa na wabunge inapotokea fedha ya Mkopo imechelewa, mkopo ambao huishia kwenye matumizi binafsi kuliko makusudio yake.
Tunavyoongea nchi inasonga mbele, ila kwa hisani ya Wakulima na Wafanyakazi, sio wasomi.
Kama hujui tofauti ya mfanyakazi na msomi mwenye kazi nitakuelewesha!

0 comments