Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula (CCM, ameahidi kushughulikia suala la ujenzi wa maegesho ya magari makubwa ya mizigo nje ya jiji la Mwanza ili kuzuia magari hayo kuingia katikati ya jiji.
Akizungumza ofisini kwake hii leo, Mabula amebainisha kuwa upo mpango wa kujenga maegesho hayo katika
maeneo yaliyo nje ya Jiji la Mwanza, hatua ambayo itasaidia magari hayo
kutoingia katikati ya Jiji na hivyo kuondoa malalamiko yaliyopo kutoka kwa madereva
wa magari madogo ya mizigo wanaolalamikia uingiaji wa magari makubwa ya mizigo
katikati ya jiji.
Ameyataja maeneo yanayotarajiwa kujengwa maegesho hao kuwa ni
Buhongwa pamoja na Igoma na kwamba baada ya ujenzi wake kukamilika, magari yote
makubwa ya mizigo hayataruhusiwa kuingia katikati ya Jiji.
Mabula ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika
uongozi uliomalizika mwaka jana, amebainisha kuwa utekelezaji wa ujenzi wa
maegesho hayo unatarajiwa kufanyika kwa uharaka zaidi ambapo amewahimiza
wawekezaji mbalimbali kujitokeza ili kushirikiana na halmashauri ya Jiji la
Mwanza kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.
Suala la magari makubwa kuingia katikati ya Jiji la Mwanza huku
yakiwa na mizigo, linalalamikiwa na madereva wa magari madogo ya mizigo kwa
kile wanachoeleza kuwa wanaingiliwa katika shughuli ambazo wao wangezifanya na
hivyo kujiingia kipato ambapo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza
kutoruhusu magari hayo kuingia katikati ya Jiji.
Bonyeza PLAY Hapa chini Kusikiliza
Bonyeza PLAY Hapa chini Kusikiliza
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari ofisini kwake.
0 comments