Sunday, 31 March 2013

NATAMANI KUONA JKT WAKIUNDA TIMU MOJA YENYE USHINDANI WA UKWELI

Na Abdallah H.I Sulayman

Msimu huu jeshi la kujenga taifa 'JKT' linatimu 4 ambazo zinashiriki ligi kuu ya vodacom, timu hizo zikiwa katika nafasi ya 7 mpaka nafasi 10 wakiwa na point 29 na yenye point chache ikiwa na point 24.

Mgambo shooting na JKT Ruvu wako katika hatihati ya kushuka daraja kama hawatachanga vizuri karata zao katika michezo ilhyosalia ya ligi kuu ya vodacom, wakati Ruvu shooting, JKT Oljoro wakiwa katika nafasi nzuri ya kubakia ligi kuu lakini kimahesabu nao wako katika uwezekano wa kushuka daraja.

Kitu kinachopelekea ligi yetu ya vodacom kukosa ladha ni kuwepo kwa thmu chache zinazoleta ushindani wa kweli katika kinyanganyiro cha ubingwa ambazo ni Simba, yanga na azam na huenda msimu ujao ikaongezeka Coastal union kama wataendelea kupata sapoti wanayopata toka kwa wadau.

Naamini JKT wanaweza wakajenga timu ya ushindani katika kinyanganyiro wa ubingwa, hivyo kuongeza ladha ya ligi kuu ya Tanzania bara na hivyo inawezekana kirahisi kama watafikia uwamuzi wa kubakia na timu moja na nguvu wanazo zitoa katika timu 4 zilizopo ligi kuu na nyinginezo zilizopo katika madaraja ya chini wakizielekeza katika timu moja na kutokubali kuwa kibaraka wa timu nyinginezo.

Natamani kujakuona timu moja ya JKT ikisimama badala ya JKT Mlale, JKT Ruvu, Mgambo JKT, Ruvu Shooting, JKT Oljoro na nyinginezo kwa maslahi ya ligi yetu.


--

MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html

0 comments