Tuesday, 9 April 2013

LINAPO KUJA SUALA LA UKABILA HAKUNA HAKI

Na Abdallah H.I Sulayman

Binadamu tumepewa udhaifu waina nyingi, moja ya udhaifu ambapo kwa jicho jingine unaweza ukasema si udhaifu ni hali ya mtu kuangalia upande wake kwanza kabla ya kuangalia upande mwingine.

Suala hilo linakuja mpaka kwenye utoaji wa hukumu kama anaetoa hukumu amelalia upande mmoja upande mwingine ni nadra kupata haki.

Suala hili la kuangalia upande wako ndio kinachotokea katika chaguzi mbalimbali za Kenya kwa kujaa ukabila katika chaguzi zao sambamba na maeneo mengine katika bara letu la Afrika.

Hapa kwetu bongo kuna makabila makubwa mawili ndani ya ulimwengu wa soka ambayo ni simba na yanga ambayo inawachukuwa asilimia 98 ya watanzania wanaopenda mchezo wa mpira wa miguu wamelalia katika makabila hayo mawili.

Ilifika kipindi katika chaguzi mbalimbali za TFF zinaangalia kabila hizo mbili na imekuwa nadra kwa vilabu vingine kupata haki zao mbele ya kabila hizo mbili, hususani katika upande wa usajili.

Kwa miaka mingi rushwa katika soka letu la bongo limekuwa tatizo kubwa na tumeshuhudia na kusikia wachezaji wakinyanganywa mpaka simu kuelekea mchezo husika, huku wachezaji wakifungiwa na vilabu vyao kwa madai wamehujumu.

Mwaka 2010 lilibuka sakata la kipa wa zamani wa Mtibwa sugar na sasa akiwa coastal union Shaban Kado kutaka kuongwa na simba akiwa mtibwa kupitia kwa mchezaji wazamani wa simba sc Ulimboka Mwakingwe na suala lao kwenda kufunikwa na polisi.

Unali kumbuka sakata lililo muweka kando mwamuzi Athumani Kazi huku wahusika wa upande wa pili wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.

Mwishoni mwa mwaka jana azam fc waliwasimamisha wachezaji wake wa 4 kwa tuhuma za kupokea rushwa na kufikishwa TAKUKURU (Taasisi ya kupambana na rushwa nchini) na kwasasa kunataarifa zimetoka TAKUKURU ya kushindwa kuthibitisha hilo kama ilivyokuwa inatarajiwa na wengi.

Sio kwamba sina imani na TAKUKURU katika utekelezaji wa shughuli zake. Wakati la wachezaji wa azam alijafika tamati limeibuka la mshambuliaji wa coastal union Nsa Job na hili tofauti na lile la wachezaji wa azam na wachezaji ambao hufungiwa kwa kosa la kuhujumu timu zao, namna TFF walivyo lichukulia.

Ni wakati wa TFF kuvua ukabila na kufuatilia mianya ya rushwa na kuwaadhibu wahusika.
--

MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html

0 comments