Wednesday, 15 May 2013

COME BACK YA MWANAHARAKATI NOVA KAMBOTA; AOMBA USHAURI WAKO?

Na Nova Kambota

Baada ya kuwa nje ya tasnia ya kublog kwa takribani miaka mitatu sasa kutokana na mizunguko ya dunia hatimaye najiandaa kurudi rasmi katika ulimwengu wa kublog ndani ya kipindi cha mwezi miezi miwili kutoka sasa.

Ikumbukwe kuwa nimeanza kublog tangu 15 Agosti mwaka 2008, hata hivyo kuna siri leo nitawamegea ndugu zangu watanzania;

-Mimi nimejaaliwa kipaji cha kuchambua maswala ya siasa
-Pia nachambua maswala ya soka
-pia nachambua maswala ya kihistoria
-Mimi pia ni mtunzi wa Riwaya
-Ni mtunzi wa mashairi
-Mwandishi wa vitabu vya kihistoria

Sasa nataka kuanzisha blog mpya ya kisasa? je nijikite kwenye nini kati ya hayo niliyoeleza hapo juu? je blog hiyo iweje?

TAFADHALI NAOMBA TOA MAONI NA USHAURI WAKO KWANGU, NAHESHIMU MAWAZO YENU MAANA BILA NYINYI NISINGEKUWA HUYU NOVA KAMBOTA MWANAHARAKATI.

Nitahakikisha nakusanya maoni yote kutoka blog zote na kuyafanyia kazi, Asante sana!

0 comments