Friday 17 May 2013

TFF YAZIMA FURSA YA KINA MESSI

Na Abdallah H.I Sulayman

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Kim Poulsein mwezi uliopita alitangaza kikosi kidogo cha timu ya Taifa (young taifa stars), kitendo ambacho kiliwashtua wapenzi wa soka nnje na wengine wakipinga kitendo hicho.

Mie nilikuwa wa mwanzo kupinga ila baada ya kupata taarifa ya ushiriki wa timu ya Taifa katika michuano ya CASTLE COSAFA CUP itakayo anza hapo baadae, lakini bila kutarajia jana TFF walithibitisha kujitoa katika michuano hiyo, ambapo Tanzania walialikwa kama ilivyo kwa Kenya.

TFF walisema wamefikia uwamuzi huo baada ya michuano hiyo kuingiliana na mchezo wa kufuzu kwa mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Uganda.

Taifa stars iliyoitwa jana ilikuwa na wachezaji 6 kati ya 24 walio itwa katika kikosi cha young Taifa stars , na hivyo kupelekea kikosi cha sasa cha Taifa stars kuwa na wachezaji 26 kati ya hao wawili ni wa kimataifa.

Hivyo basi wachezaji 24 waliosalia ni wachezaji wenye sifa ya kucheza dhidi ya Uganda katika mchezo wa kufuzu CHAN.

Je kocha Poulsein atawatumia wapi kati ya Taifa stars na young taifa stars?

Asilimia zaidi ya 80 nina amini Poulsein atawatumia Taifa stars katika mchezo huo dhidi ya Uganda na hapo ndipo ninapo ona hakukuwa na tija kwa TFF kuichomoa Tanzania katika michuano ya COSAFA wakati kuna young taifa stars ambayo inahitaji michezo ya kimataifa ili kuwa weka vizuri kwa ajili ya kuchukuwa nafasi za wachezaji wa Taifa stars.

Kwa ufupi naweza sema TFF wamezima fursa ya kina Messi wa Simba na Coastal union (Ramadhani Singano na Twaha Ibrahim), Casilasi wa Mtibwa sugar (Husein Sharif), Miraji na wengineo walio jumuishwa katika young taifa stars kutamba kimataifa.

Bado TFF hawajanitosheleza kwa sababu walizotoa kwa kudhibitisha kutoshiriki kwa Tanzania katika michuano hiyo ya COSAFA, wakati tumeshuhudia mara ngapi timu za Zambia, Malawi kuleta timu zao B katika michuano ya CECAFA pale wanapo alikwa.

KWA HALI HII YOUNG TAIFA STARS HAINA TIJA.

0 comments