Friday, 24 May 2013

JAMAA ALIPOLETA KUJUANA JESHINI

Jamaa alipita sehemu isiyoruhusiwa katika kambi ya jeshi  na akapewa adhabu ya kuhamisha matofali 1000! Jamaa akajitahidi akabeba matofali 900 na akawa hoi! Na ghafla akakumbuka kuwa mkuu wa kambi hiyo ni rafiki yake na wamesoma wote.

Jamaa akampigia simu mkuu wa kambi;
Jamaa "Mkuu, vijana wako wamenipa adhabu ya kuhamisha matofali 1000".
Mkuu "hao wajinga kweli hawajui tunavyofahamiana! Wasikusumbue mi ndo mkuu wao. Zirudishe palepale zilipokuwa mwanzo halafu uje ofisini tuonane". 

0 comments