Friday, 10 May 2013

PONDA: MAPAMBANO YANAENDELEA

Shekhe Issa Ponda leo baada ya swala ijumaa, amezungumza na waislamu kwa mara ya kwanza toka atoke jela hapo jana katika msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es salaam.

Shekhe Ponda katika hotuba yake leo amesema mapambano ya kutetea haki za waislamu yataendelea mpaka dhulma iliyokidhiri ndani ya serikali ya Tanzania dhidi ya uislamu utakapo fikia kikomo.

Shekhe Ponda alifafanua baadhi ya dhulma wanazotendewa waislamu katika nchi hii ya Tanzania, huku akisisitiza kuwa hawezi kuondolewa nchini hapa na kifo kitamkutia humu humu.

Shekhe Ponda aliwashukuru waislamu kwa ushirikiano waliouonyesha kwake, huku hakisisitiza umoja uliopo udumu katika mapambano ya kusaka haki.

0 comments