Thursday, 30 May 2013

Rasimu ya Katiba kuzinduliwa Jumatatu, Juni 3, 2013

Na   Assaa Rashid

Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa itafanya uzinduzi wa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumatatu, Juni 3, 2013, kuanzia saa 8:00 mchana  katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utarushwa moja kwa moja na vituo vya redio vya TBC Taifa, ZBC Redio na vituo vya televisheni vya TBC 1 na ZBC TV na vituo vinginevyo vya redio na televisheni.
Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, ujumbe mfupi wa simu za mikononi (sms) na nyinginezo.
Tume inawaomba wananchi na wadau kufuatilia uzinduzi huo kwa makini kupitia vyombo hivyo vya habari.
Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Alhamisi, Mei 30, 2013 

0 comments