Tuesday, 21 May 2013

TANZANIA BARA KUWAKILISHWA NA SIMBA NA YANGA KAGAME

Na Abdallah H.I Sulayman

Habari za siku wapendwa mashabiki wenzangu wa azam fc sambamba na wale wafuatiliaji wa soka la bongo ambapo limegawanywa katika makabila makubwa mawili ya Simba na yanga.

Kuna maswali yamekuwa yakinifikia kama blogger wa blog ya www.azamfans.blogspot.com kuhusu timu zipi zitakazo shiriki michuano ya Kagame Cup yanayotaraji kuanza juni 18 nchini Sudan Kusini. Wengi wakiuliza kama azam fc watashiriki?

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo ya Klabu bingwa Afrika mashariki na kati 'Kombe la Kagame';
1. Ni kuwa kila nnchi mwanachama wa CECAFA (Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati) itawakilishwa na bingwa wa ligi kuu ya nchi husika.

Tanzania bara pamoja na Zanzibar huwangalia bingwa wa msimu mmoja nyuma (bingwa atakae iwakilisha Tanzania bara na Zanzibar ni mabingwa wa msimu wa 2011/12 na wala si bingwa wa msimu wa 2012/13 ambao teyari wamesha patikana), hivyo basi Tanzania bara atawakilishwa na simba sc na upande wa Zanzibar utawakilishwa na Super falcon.

2. Nnchi mwenyeji anapata fursa moja ya upandeleo wa kuongeza timu ambayo huchukuliwa na makamu bingwa wa nnchi hiyo, hivyo basi Sudani Kusini atawakilishwa na timu mbili.

Bingwa mtetezi wa kombe la Kagame hupata nafasi ya moja kwa moja kutetea kombe lake na ikitokea bingwa mtetezi akawa miongoni mwa mabingwa wa nchi mwanachama, basi makamu bingwa wa nchi husika (timu iliyoshika nafasi ya katika nchi ambaye bingwa wake ni bingwa mtetezi) atapata fursa.

Yanga ataingia katika michuano hiyo kwa tiketi ya bingwa mtetezi na wala si bingwa wa Tanzania bara, wakati Simba wanaingia kwa tiketi ya ubingwa wa Tanzania bara.

4. Ikitokea bingwa mtetezi akatoka katika nchi mwenyeji basi nchi husika itawakilishwa na timu 3, moja kwa tiketi ya bingwa wa nchi, wapili kwa tiketi ya bingwa mtetezi na yatatu kwa tiketi ya uwenyeji. Hii hali ilitokea mwaka jana pale Tanzania Bara ilipowakilishwa na Yanga kama bingwa mtetezi, Simba nafasi ya ubingwa wa nchi (yanga ndie aliyekuwa bingwa wa msimu wa 2010/11, wakati simba akiwa nafasi ya pili) azam fc nafasi ya uenyeji wa mashindano.


Kwa mujibu wa taarifa zilizotufika timu 13 zimethibitisha kushiriki ambapo Simba na yanga ni miongoni mwa hizo 13 sambamba na Super falcon.

0 comments