Saturday, 1 June 2013

MAKANISA MATUPU NA MISIKITI YAFURIKA

Na MIMI NI MUISLAMU, FACEBOOK

Namba sensa na hali halisi vyathibitisha ya kuwa uislamu ndio dini ya miaka ijayo ya Uingereza.
Gazeti la Dail mail la nchini Uingereza katika toleo lake la siku ya alkhamisi 30/5/­2013,lilisambaza takriri juu ya kukua kwa uislamu nchini Uingereza.


Gazeti hilo likaonesha picha kwa kulinganisha idadi ya waislamu wanao hudhuria misikitini na idada ya wakristo wanao hudhuria makanisani.


Likathibitisha ya kuwa idadi ya waislamu wanao hudhuria misikitini ya ipita mara dufu idadi ya wakristo wanao hudhuria makanisani.


Gazeti hilo likasema ya kuwa,huenda ipo siku kanisa la St George litafurika kwa mara nyingine waswaliji,lakini wanaweza kuwa si wasristo.


Gazeti likaendelea kusema ya kuwa,ukiwa unataka kuiona dini ya leo nchini Uingereza,basi tosheka na kuiangalia picha hii.


Kwani picha ni dalili tosha kulikoni sensa rasmi ya aina yoyote. Picha hii yaonesha utekelezaji wa ibada ya waislamu na wakristo mashariki mwa Uingereza.

Gazeti lilionesha picha mbili za kanisa la St George na kanisa la St Mary, ama picha ya tatu ni picha ya waislamu wakiwa wanaswali nje ya msikiti.


Gazeti likaendelea kusema ya kuwa waweza ona tofauti kubwa kati ya msikiti na kanisa. Katika kanisa la kwanza St George lililo jengwa karne ya 18 lenye kuingiza watu zaidi ya Alfu moja,linaonekana likiwa na kiasi cha watu 12 basi walio elekea kutekeleza ibada.


Vile vile kanisa la St Mary linaonesha ambalo linaonesha likiwa na kiasi cha watu 20 ndani yake kama inavyo dhihiri katika picha.Picha ambazo zimepigwa katika ibada ya siku ya jumapili.


Muda ambao makanisa ni matupu kabisa , kinyume cha misikitini ya kukodiwa,misikiti ambayo ukubwa wake haulingani na ukubwa wa chumba kimoja cha kanisa,misititi ambayo imekuwa haina uwezo wa kuingiza watu zaidi ya mia moja.Waislamu wamekuwa wakifurika na idadi yao imekuwa ikiongezeka mara dufu siku ya ijumaa hali ambayo imewapelekea wawe wakiswali nje katika mitaa inayo karibiana na msikiti.

Gazeti la Dail Mail limemalizia kwa kusema ya kuwa Ukristo umekuwa ni dini ya zamani na Uislamu ndio dini ya mustakbali nchini Uingereza.


Chanzo:  http://www.dailymail.co.uk/news/article-2332998/One-country-religions-telling-pictures-The-pews-churches-just-yards-overcrowded-mosque.html

0 comments